Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya kitengo cha ubaguzi Taasisi ya Kituruki ya Kiislamu na Masuala ya Kidini (DITIB) yenye makao yake makuu katika mji wa kaskazini wa Cologne. Taarifa hiyo imebaini kuwa barua nyingi na barua pepe zenye matusi na vitisho zimetumwa kwenye misikiti nchini Ujerumani.
Msikiti wa Kati wa Cologne pekee umepokea barua pepe na barua kwa njia ya posta 17, na hivi karibuni zaidi, Msikiti wa DITIB Selimiye katika mji wa kaskazini wa Dinslaken ulilengwa.
Kutokana na hali hii, Waislamu Ujerumani wanazidi kuwa na wasiwasi.
Mwezi uliopita, msikiti mmoja katika mji wa Munster magharibi mwa Ujerumani pia ulipokea barua ya vitisho iliyokuwa na matusi dhidi ya Waislamu na wahajiri.
Pia ilikuwa na matamshi ya kibaguzi, ikiwa ni pamoja na "Ujerumani kwa Wajerumani, wageni nje."
Mkuu wa Jumuiya ya Msikiti wa Munster Central, Fettah Cavus, alisema kuwa kwa masikitiko, chuki dhidi ya wageni na Waislamu inaongezeka nchini Ujerumani.
3486859